|
|
|
- Kuwa mtu anayeheshimu watu. Kuwa mtu anyefanya juhudi ya kuielewa, kuieleza, kuitetea, na kuitekeleza itikadi na siasa ya CCM. Kuwa mtu mwenye kuamini kuwa kazi ni kipimo cha utu, na kuitekeleza imani hiyo kwa vitendo.
.
- Kuwa mtu anayependa kushirikiana na wenzake. Kuwa mbu ambaye siku zote yuko mstari wa mbele katika utekelezaji wa mambo yote ya umma, kulingana na miongozo ya CCM.
.
- Kuwa wakati wote ni mfano wa tabia nzuri kwa vitendo vyake na kauli yake, kuwa mwaminifu, na kutokuwa mlevi au mzururaji. Kuwa ama mkulima, mfanyakazi au mwenye shughuli nyingine yoyote halali ya kujitegema.
.
- Mtu atakayetaka kuwa mwanachama atajaza karatazi maalum ya maombi na kuipeleka kwa Katibu wa Tawi anapoishi Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Tawi itafikiria na kutoa uamuzi wa mwisho kuhusu maombi ya uanachama.
.
- CCM kitakuwa na mpango wa kutoa mafunzo kwa wanachama wake juu ya imani, malengo na madhumuni ya siasa ya CCM kwa jumla.
.
- Mtu akikubaliwa kuwa Mwanachama itabidi atekeleze haya yafuatayo: Atatao kiingilio cha Uanachama atalipa ada ya Uanachama kila mwezi isipokuwa kama akipenda kulipa ada ya waka mzima mara moja.
.
- Atatoa michango yoyote itakayoamuliwa Viwango vya kiingilio, ada na michango vitawekwa na Halmasharui Kuu ya Taifa.
.
- Uanachama wa mwanachama utakwisha kwa ama:- Kujiuzulu mwenyewe; Kuachishwa kwa mujibu wa Katiba Kufukuzwa kwa mujibu wa Katiba Kutotimiza mashari ya uanachama; au Kujiunga na Chama kingine chochote cha siasa.
.
- Mwanachama ambaye uanachama wake unakiwsha kwa sababu yoyote ile hatarudishiwa kiingilio alichokitoa, ada aliyotoa wala michango yoyote aliyoitoa. Itabidi arudishe Kadi ya Uanachama wa CCM.
.
- Mwanachama aliyeachishwa au kufukuzwa Uanachama akitaka tena kuingia katika CCM itabidi aombe upya, na atapeleka maombi yake hayo ama katika Halmashauri Kuu ya wilaya au kikao kilichomwachisha au kumfukuza Uanachama.
.
- Mwanachama aliyejiuzulu akitaka kuingia tena katika CCM ataomba upya kwa kufuata utaratibu wa kuomba Uanahcama kwa mujibu wa Katiba ya CCM.
|
|
|