RATIBA YA ZOEZI LA KUWAPATA WAGOMBEA WA CCM KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA VIJIJI NA VITONGOJI – TANZANIA BARA MWAKA 2004
1.0 UTANGULIZI
1.1 Kwa kuzingatia ratiba ya Wizara ya Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa iliyotolewa kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vitongoji na Vijiji mwaka 2004; na kwa kuzingatia Katiba ya CCM toleo la 1997 ambayo inaelekeza taratibu za CCM kwa chaguzi hizo kupitia vikao vya kutoa maoni, kuchuja, kupendekeza na hatimaye kufanya uteuzi wa mwisho kwa mujibu wa Ibara 27:3; 34:4(e); 37:8(e); 39:5(b-c) na 49:6(c); Chama Cha Mapinduzi Makao Makuu kimeandaa Ratiba ya kuzingatiwa.
1.2 CCM imedhamiria kwa mara nyingine kushinda kwa kishindo Vitongoji, Mitaa na Vijiji vyote nchi nzima. Hilo ndilo lengo la CCM na ni vema lizingatiwe. Ushindi mkubwa utakaopatikana katika uchaguzi wa Vitongoji, Mitaa na Vijiji utaijengea CCM msingi imara wa kushinda kwa kiwango cha juu katika uchaguzi Mkuu wa 2005.
2.0 KURA ZA MAONI
2.1 Utaratibu wa CCM kuwapata wagombea wake ni wa kupitia kura za maoni. Hivyo baada ya kuzingatia ratiba ya Serikali taratibu zilizoandaliwa ndani ya CCM zinatoa fursa ya kushiriki uchaguzi huo na kushughulikia malalamiko yatakayojitokeza kabla ya siku ya kuchukua fomu za Serikali zitakazotolewa kuanzia tarehe 28/10/2004.
2.2 Ratiba ya taratibu za kura za maoni, uchujaji na uteuzi wa Wagombea wa CCM iwe kama ifuatavyo kwa Mikoa yote Tanzania Bara:-
- Tarehe 20-26/9/2004 Waombaji uongozi kuchukua na kurejesha fomu kwa Katibu wa CCM wa Tawi. (Kurejesha tarehe 26/9/2004 kabla ya saa 10 jioni).
- Tarehe 28/9/2004 – 2/10/2004 Kura za Maoni ngazi za Vitongoji, Mitaa.
- Tarehe 3-7/10/2004 Kura za Maoni ngazi ya Vijiji.
- Tarehe 9/10/2004 – 13/10/2004 Vikao vya Kamati za Siasa za Matawi kuchuja na kupendekeza majina ya waombaji wa Vitongoji, Mitaa na Vijiji.
- Tarehe 15/10/2004 – 18/10/2004 vikao vya Halmashauri Kuu za Matawi
(a) Kuteua majina ya wagombea Uongozi wa Vitongoji na Mitaa.
(b) Kupndekeza majina ya waombaji uongozi wa Serikali za Vijiji na kuwasilisha mapndekezo hayo kwenye Kata..
- Tarehe 20/10/2004 – 26/10/2004 vikao vya Kamati za Siasa za Kata kuteua majina ya wagombea nafasi za Uongozi wa Serikali za Vijiji na kurejesha majina kwenye Matawi.
- Tarehe 28/10/2004 – 30/10/2004 wagombea uongozi walioteuliwa na Chama kugombea Uongozi wa Vitongoji, Mitaa na Vijiji kuchukua fomu za uteuzi za Uchaguzi kwa wasimamizi wa uchaguzi wa Serikali.
- Tarehe 1-2/11/2004 CCM kuhakiki Ujazaji wa fomu za wagombea na kuzirudisha kwa wasimamizi wa Uchaguzi wa Serikali.
- Tarehe 4/11/2004 Wasimamizi wa Uchaguzi wa Serikali kuteua majina ya wagombea uongozi wa Mitaa, Vitongoji na Vijiji.
- Tarehe 3-5/11/2004 Uteuzi wa Mawakala wa CCM.
- Tarehe 5/11/2004 CCM kuwasilisha pingamizi au malalamiko dhidi ya uteuzi kwa wasimamizi wa uchaguzi wa Serikali (kama ipo haja ya kufanya hivyo).
- Tarehe 8/11/2004-19/11/2004 Kampeni za Uchaguzi.
- Tarehe 21/11/2004-27/11/2004 Uchaguzi wa Viongozi wa Vitongoji na Mitaa.
- Tarehe 28/11/2004 Uchaguzi wa Viongozi wa Vijiji.
3.0 RATIBA YA KUZINGATIWA KATIKA KUWAPATA WAGOMBEA WA CCM KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, VIJIJI NA VITONGOJI MWAKA 2004
NA. | TAREHE | SHUGHULI | MHUSIKA AU WAHUSIKA |
1. | 20-26/9/2004 | Uchukuaji wa fomu za Uongozi wa Vitongoji,Mitaa na Vijiji | Makatibu CCM wa Matawi na Kata |
2. | 26/9/2004 | Urejeshaji wa fomu za Uongozi kwa Katibu wa Tawi kwa ngazi za Vitongoji, Mitaa na Vijiji. (kabla ya saa 10.00 jioni). | Wagombea wote Makatibu wa CCM wa Matawi na Kata. |
3. | 28/9/2004 -2/10/2004 | Kura za Maoni kwa Wagombea Uongozi Ngazi ya Vitongoji na Mitaa | Kamati za Siasa za Matawi na Kata |
4. | 3-7/10/2004 | Kura za Maoni kwa Wagombea Uongozi Ngazi ya Vijiji | Kamati ya Siasa za Matawi, Kata na Wilaya |
5. | 9-13/10/2004 | Vikao vya Mapendekezo kuhusu Wagombea wa Vitongoji, Mitaa, Vijiji na Wajumbe wa Serikali za Vijiji na Mtaa | Kamati za Siasa za Matawi |
6. | 15-18/10/2004 | (a) Vikao vya uteuzi kwa nafasi ya Wenyeviti wa Vitongoji, Mitaa na Wajumbe wa Serikali za Mitaa.
(b) Kutoa mapendekezo ya wagombea ngazi ya Vijiji. |
Halmashauri Kuu za Matawi |
7. | 20-26/10/2004 | Vikao vya Uteuzi wa mwisho kwa nafasi za Wenyeviti na Wajumbe wa Serikali za Vijiji. | Kamati za Siasa za Kata |
8. | 28-30/10/2004 | Siku ya kuchukua fomu za uteuzi kwa Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali | 1. Mgombea wa CCM
aliyeteuliwa kwa kila nafasi 2. Makatibu wa CCM wa Matawi na Kata. |
9. | 1-2/11/2004 | Kuhakiki fomu za Wagombea na kuzirudisha kwa Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali | 1.Mgombea
aliyeteuliwa 2.Makatibu wa CCM wa Matawi na Kata. |
10. | 4/11/2004 | Wasimamizi wa Uchaguzi kuteua majina ya wagombea | Wasimamizi wa Uchaguzi wa Serikali |
11. | 3-5/11/2004 | Uteuzi wa Mawakala wa CCM | Kamati za Siasa za Matawi na Kata |
12. | 5/11/2004 | Kuwasilisha pingamizi/Malalamiko dhidi ya Uteuzi kwa Msimamizi wa Uchaguzi | Wagombea wa CCM walioteuliwa |
13. | 8-19/11/2004 | Mikutano ya Kampeni za Uchaguzi | Kamati za Siasa za Matawi na Kata. |
14. | 21/11/2004 | Uchaguzi wa Viongozi wa Vitongoji na Mitaa. | – Makatibu CCM Kata
na Matawi – Wasimamizi wa Uchaguzi |
15. | 28/11/2004 | Uchaguzi wa Viongozi wa Vijiji. | -Makatibu wa CCM wa Kata na Matawi
-Wasimamizi wa Uchaguzi. |
KIAMBATISHO
RATIBA ILIYOTOLEWA NA SERIKALI ZA MITAA NA TAWALA ZA MIKOA KUHUSU UTEKELEZAJI WA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA NGAZI ZA VIJIJI, VITONGOJI NA MITAA KWA MWAKA 2004
NA. | TAREHE | SHUGHULI | MHUSIKA AU WAHUSIKA |
1. | 29/1-29/2/2004 | ORTAMISEMI kufanya mapitio ya Kanuni za Uchaguzi za 1999 na kuandaa mapendekezo | ORTAMISEMI |
2. | 20/3-28/3/2004 | ORTAMISEMI kuandaa makisio ya gharama ya uchaguzi na kuwasilisha Hazina | ORTAMISEMI |
3. | 17/4/2004 | ORTAMISEMI kuandaa na kuendesha mkutano na viongozi wa Kitaifa wa vyama vya Siasa | ORTAMISEMI |
4. | 10/6-24/6/2004 | ORTAMISEMI kuandaa na kuendesha mkutano wa Wadau (Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Tume ya Uchaguzi, Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya) | ORTAMISEMI |
5. | 25/6-31/7/2004 | ORTAMISEMI kuandaa na kuendesha mkutano wa Wadau, Wakurugenzi wa Halmashauri na Mameya/Wenyeviti | ORTAMISEMI |
6. | 21/8/2004 | Waziri kutoa Tangazo kwa umma kuhusu Uchaguzi | WAZIRI |
7. | 24/8-6/9/2004 | Wasimamizi Wasaidizi kuandaa orodha za wapiga kura kutoka kwenye rejesta ya wakazi | WASIMAMIZI WASAIDIZI WA UCHAGUZI |
8. | 23/8-1/9/2004 | ORTAMISEMI kuandaa mada za kufundishia Wasimamizi wa Uchaguzi | ORTAMISEMI |
9. | 6/9/-13/9/2004 | Wasimamizi kubandika orodha ya Wapiga Kura | WASIMAMIZI WASAIDIZI WA UCHAGUZI |
10. | 9/9-13/9/2004 | Wasimamizi wa Uchaguzi kupokea na kusikiliza pingamizi dhidi ya orodha ya wapiga kura | WASIMAMIZI WASAIDIZI WA UCHAGUZI |
11. | 4/9-18/9/2004 | – ORTAMISEMI kupokea vifaa vya uchaguzi toka kwa Mpiga Chapa wa Serikali/Wazabuni wengine
– Kununua vifaa visivyopatikana kwa Mpiga Chapa wa Serikali. |
ORTAMISEMI |
12. | 19/9-8/10/2004 | ORTAMISEMI kusafirisha vifaa vya uchaguzi kwenda kwenye Halmashauri | ORTAMISEMI |
Wasimamizi wa Uchaguzi kuendesha Semina za Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi | WASIMAMIZI WA UCHAGUZI | ||
13 | 9/10-23/10/2004 | Msimamizi wa Uchaguzi kusambaza vifaa vya uchaguzi kwenye Vijiji, Mitaa na Vitongoji | WASIMAMIZI WA UCHAGUZI |
14. | 23/10/2004 | Wasimamizi wa Uchaguzi kutoa maelekezo ya uchaguzi | WASIMAMIZI WA UCHAGUZI |
15. | 28/10-4/11/2004 | Katibu Tawala wa Mkoa kuteua Kamati ya Rufaa | KATIBU TAWALA WA MKOA |
Siku ya kuchukua na kurudisha fomu za uteuzi | WASIMAMIZI WA UCHAGUZI | ||
16. | 4/11/2004 | Siku ya uteuzi | WASIMAMIZI WA UCHAGUZI |
17. | 5/11/2004 | Kuwasilisha pingamizi malalamiko dhidi ya uteuzi | WASIMAMIZI WASAIDIZI WA UCHAGUZI |
18. | 6/11-7/11/2004 | Kusikiliza malalamiko/pingamizi ya uteuzi | WASIMAMIZI WASAIDIZI WA UCHAGUZI |
19. | 8/11-19/11/2004 | Mikutano ya Kampeni | WAGOMBEA |
20. | 20/11/2004 | Wasimamizi wa Uchaguzi kutoa tangazo la mdomo juu ya uchaguzi kesho yake 21/11/2004 | WASIMAMIZI WA UCHAGUZI |
21. | 21/11/2004 | Siku ya Uchaguzi wa Vitongoji. | – WAPIGA KURA
-WASIMAMIZI WA UCHAGUZI |
22. | 27/11/2004 | Wasimamizi wa Uchaguzi kutoa taarifa ya mdomo juu ya Uchaguzi wa Vijiji | WASIMAMIZI WA UCHAGUZI |
23. | 28/11/2004 | Siku ya Uchaguzi wa Vijiji na Mtaa | – WAPIGA KURA
– WAGOMBEA – MSIMAMIZI WA UCHAGUZI |
24. | 6/12-11/12/2004 | Kuitishwa kwa mikutano ya kwanza ya Halmashauri mpya za vijiji na Kamati za Mitaa | MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA WENYEVITI WA MITAA |